Dkt. Taqavi alifafanua kuwa Bibi Zainab (sa) ni kioo cha ukamilifu wa mwanamke wa Kiislamu, aliyelelewa katika malezi bora ya Mtume Mtukufu (saww) na Imam Ali (as), na akapata elimu ya kimbinguni kutoka kwao. Alikuwa mshauri wa karibu wa Maimamu watatu watukufu - Imam Hassan (as), Imam Hussein (as), na Imam Sajjad (as), na msaada mkubwa kwa Imam Sajjad (as) baada ya tukio la Ashura.

27 Oktoba 2025 - 15:51

Hawzat Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni | Hafla ya Kuzaliwa kwa Bibi Zainab (sa) Yaadhimishwa Kwa Shangwe

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, 27 Oktoba 2025, Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) - Dar-es-Salaam, Tanzania, Dkt. Ali Taqavi, leo tarehe 27 Oktoba 2025, amekutana na wanafunzi mabinti wa Hawzat Hazrat Zainab (sa) iliyopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam, katika hafla adhimu ya kusherehekea kuzaliwa kwa Bibi Zainab (sa) - binti mpenzi wa Imam Ali bin Abi Talib (as) na mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Hawzat Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni | Hafla ya Kuzaliwa kwa Bibi Zainab (sa) Yaadhimishwa Kwa Shangwe

Katika hotuba yake ya kipekee, Dkt. Taqavi alisisitiza nafasi na daraja tukufu la Sayyidat Zainab (sa) katika historia ya Uislamu, akieleza kwamba: “Masaibu ya Bibi Zainab (sa) ni magumu mno kuyazungumzia; yanagusa moyo wa kila muumini. Yamebeba mafunzo makubwa kwa wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) kuhusu subira, imani na ujasiri.”

Dkt. Taqavi alifafanua kuwa Bibi Zainab (sa) ni kioo cha ukamilifu wa mwanamke wa Kiislamu, aliyelelewa katika malezi bora ya Mtume Mtukufu (saww) na Imam Ali (as), na akapata elimu ya kimbinguni kutoka kwao. Alikuwa mshauri wa karibu wa Maimamu watatu watukufu - Imam Hassan (as), Imam Hussein (as), na Imam Sajjad (as), na msaada mkubwa kwa Imam Sajjad (as) baada ya tukio la Ashura.

Hawzat Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni | Hafla ya Kuzaliwa kwa Bibi Zainab (sa) Yaadhimishwa Kwa Shangwe

Akiendelea, aliongeza kuwa Sayyidat Zainab (sa) ni mfano bora wa subira na uvumilivu:

“Ukitaka kujifunza subira ya kweli, jifunze kutoka kwa Bibi Zainab (sa). Alivumilia masaibu makubwa ya Karbala kwa moyo wa imani na ujasiri wa hali ya juu.”

Aidha, Dkt. Taqavi aliwahimiza wanafunzi mabinti wa Hawza hiyo kuendeleza maadili na heshima ya Kiislamu kupitia vazi la Hijabu na mwenendo mwema, akisema: “Hijabu yenu iwe ni hijabu ya Sayyidat Zainab (sa), na akhlaq zenu ziwe akhlaq za Ahlul-Bayt (as). Mnaishi katika jamii yenye changamoto nyingi kwa mabinti wa Kiislamu, hivyo ni wajibu wenu kupambana ili kulinda maadili ya dini.”

Hawzat Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni | Hafla ya Kuzaliwa kwa Bibi Zainab (sa) Yaadhimishwa Kwa Shangwe

Alionya kuwa maadui wa Uislamu hawapendi kuona binti wa Kiislamu akizingatia heshima ya Hijabu, akisisitiza kuwa ni wajibu kwa kila muumini kufanya jihadi kubwa ya kimaadili katika kulinda mafunzo ya Kiislamu na thamani za Ahlul-Bayt (as).

Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Dkt. Taqavi aligusia chuki na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya maadui wa Ahlul-Bayt (as) wanaokashifu makaburi matukufu, akieleza kuwa wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) wanaamini katika shafaa – uombezi wa Mtume (saww) na kizazi chake kitakatifu – kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. “Ni itikadi yetu kuwa Mtume (saww) na Ahlul-Bayt wake (as) wanayo nafasi ya uombezi mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Kiyama. Hii ni imani safi ya wafuasi wa Ahlul-Bayt (as), na hakuna sababu ya matusi au fedheha dhidi ya watukufu wa dini.”

Hawzat Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni | Hafla ya Kuzaliwa kwa Bibi Zainab (sa) Yaadhimishwa Kwa Shangwe

Hafla hii imehitimishwa kwa dua maalum, nyimbo za mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as), na pongezi kwa wanafunzi wote wa Hawzat Hazrat Zainab (sa) walioandaa maadhimisho haya kwa uzuri na nidhamu.

Hawzat Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni | Hafla ya Kuzaliwa kwa Bibi Zainab (sa) Yaadhimishwa Kwa Shangwe

Your Comment

You are replying to: .
captcha